Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Serengeti Bi. Rebeca Msambusi amewataka walimu wote waliohamishiwa katika shule mpya za Sekondari kuwa na subira juu ya stahiki zao za uhamisho.
Ameyasema hayo leo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa kawaida wa baraza la Madiwani, mkutano ambao ni wa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019
Kabla ya kujibu swali hilo la msingi kutoka kwa Mh. Diwani wa Kata ya Sedeco, Bi. Rebeca alianza kwa kuwashukuru Waheshimiwa madiwani kwa ushirikiano wao.
“Tunawashukuru waheshimiwa madiwani ambao wameshirikiana kwa ukaribu na menejimenti kuhakikisha zile shule saba mpya za sekondari zinakamilika na kuweza kufunguliwa” amesema Bi. Rebeca
Akizungumzia juu stahiki za uhamisho amesema kuwa shule hizo zilikuwa zimeshafunguliwa na ilikuwa ni lazima kuwapeleka walimu ili ziweze kufanya kazi.
“Lakini baada ya kufunguliwa ilibidi tupeleke walimu ili zianze kufanya kazi ni dhahiri Muheshimiwa Mwenyekiti tunatambua stahiki zao na zimeshafanyiwa hesabu na zinafahamika katika Menejimenti na kinachobakia sasa hivi tunasubiria fedha za ruzuku tuweze kuwalipa” Alijibu Bi Rebeca
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019 Halmashauri imeweza kukamilisha na Kuzifungua shule mpya saba (7) ambapo walimu wapatao 37 waliamishishiwa katika shule hizo mpya na kwa ujumla walimu hao wanadai jumla ya Tsh. 93,000,000/= (Milion tisini na tatu) ikiwa ni stahiki zao za uhamisho kwenda katika vituo hivyo vipya.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti