Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma (Diwani wa kata ya Busawe) akiwa ameambata na Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti na Baadhi ya wataalamu wamefanya ziara ya kutembelea hifadhi ya serengeti kwa nia ya kuhimiza utalii na utunzaji wa mazingira.
Akizungumza katika shule ya Mazingira Mhe makuruma amewakumbusha madiwani kuwa ziara hiyo inalengo la kujionea shughuli za kiuhifadhi na kitalii zinazofanywa na Kampuni ya Grumeti reserves sambamba na kuhimiza utalii kwa kuweza kujionea wanyama mbalimbali katika hifadhi hiyo kubwa ya Serengeti.
‘’Madiwani hawa ni wawakilishi wa wananchi kutoka katika Kata 30, kwahiyo ujumbe na kazi mnazozifanya zitawafikai wananchi kupitia madiwani hawa,lakini pia naamini mahusiano yatakwenda kuwa mazuri Zaidi kwa sababu wananchi hawa watajionea na kutambua kazi gani mnazifanya’’alisema makuruma
Aliongeza pia kutokana na ziara hiyo itakuwa chachu ya kuwahimiza wananchi kutunza mazingira na kuachana na vitendo hatarishi vinatavyoopelekea hifadhi hiyo kuathirika.
Kwa upande wa TAWA wameomba madiwani hao kuwiwa na kuchukua hatua za kiuhifadhi na kulinda mazingira ya hifadhi kwa ajili ya ustawi ya Jamii na kupiga vita vitendo vya kijangili.
Aidha,Madiwani hao wamemshukuru mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Mhe.Ayub Makuruma kwa kuona umuhimu wa kutembelea hifadhi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono Juhudi za Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuhimiza utalii,lakini pia kupata nafasi ya kujifunza kazi kubwa anayoifanya muwekezaji huyo katika hifadhi ya Serengeti.
Madiwani wamepata nafasi ya kutembela vitalu vya uwindaji na utalii ambavyo muwekezaji wake Kampuni ya Grumeti Reserves imewekeza amabavyo ni Ikorongo,Grumeti na IKONA WMA.Pori la akiba la Ikorongo na IKONA WMA lipo Wilayani Serengeti lakini Kitalu cha Grumeti kuna upande lipo Wilaya ya Bunda na upande lipo katika wilaya ya Serengeti.
Uwekezaji huo umekuwa na manufaa makubwa kwa Wananchi wanaoishi kwatika wilaya ya Serengeti ikiwemo kusaidia katika shughuli mbalimbali za kimaendeleao,ufadhili wa masomo ambao unafanyika chini ya idara ya maendeleo ya Jamii inayongozwa na Bi. Frida Mollel. Vile vile madiwani hao walipata nafasi ya kushuhudia mifumo ya kisasa ya kiteknolojia za kimawasiliano, kiusalama dhidi ya majangili na uzuiaji wa wanyama hatarishi wanapoingia katika makazi ya binadamu.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti