Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanya kikao cha Baraza la Madiwani la uwasilishaji wa taarifa za utekelezajkali wa kata kwa robo ya kwanza (Julai - Septemba 2023) ambapo kwa mara ya kwanza taarifa hizo zimewasilishwa na watendaji wa kata kwa niamba ya madiwa wa kata husika.
Katika kikao kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti ambaye pia ni diwani wa kata ya Busawe Mhe. Ayub M. Makuruma, kwa kauli moja madiwani wameridhia taarifa hizo ziwasilishwe na watendaji wa kata.
Baada ya watendaji wa kata kuwasilisha taarifa hizo waheshimiwa madiwani walipata nafasi ya kutoa mapendekezo na ushauri kuhusu namna ya utatuzi wa changamoto mbalimbali katika kata na kushauri namna bora ya usimamizi na utekelezaji miradi mbalimbali katika kata zao.
Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg. Afraha N. Hassan ameaidi kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na kufanyia kazi ushauri na maelekezo yaliyotolewa na Baraza la madiwani.
Baraza la Madiwani litaendelea siku ya kesho ambapo utakuwa ni Mkutano wa wazi huku kamati mbalimbali zikiwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zilizofanywa na Halmashauri kwa kipindi chote cha robo ya Kwanza (Julai - Septemba 2023)
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti