Halmashauri ya wilaya ya Serengeti kupitia Idara ya afya, Leo Juni 7, imezindua Kampeni ya Mwezi wa Afya na Lishe ya Mtoto yenye lengo la kuimarisha afya za watoto nchini.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Serengeti Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Adam Lusubilo kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji amesema, Halmashauri itahakikisha inashiriki kikamilifu katika kusimamia na kutekeleza afua zote za lishe ili kuimarisha afya za watoto huku akiwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kikamilifu.
Kwa upande wao, wananchi waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo, wameishukuru serikali kwa kuanzisha Kampeni hii kwani itasaidia kuimarisha afya za watoto sambamba na kupunguza gharama za matibabu ya mtoto pale anapokosa lishe bora.
Kampeni ya mwezi wa afya na lishe ya mtoto hufanyika mara mbili katika kipindi cha mwaka mmoja kwa mwezi wa 6 na mwezi wa 12 ikiwalenga watoto wenye umri wa miezi 6 hadi miezi 59.
Aidha, katika kampeni hiyo hutolewa matone ya vitamini A, utoaji wa dawa za minyoo, utambuzi wa hali ya lishe sambamba na utoaji wa Elimu ya Afya na lishe ambapo katika Wilaya ya Serengeti huduma hizi hutolewa katika Zahanati zote, Vituo vya Afya na Hospitali zote.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti