Kijiji cha Iharara ni moja kati ya vijiji 78 vinavyopatikana Halmashauri ya Serengeti 14/02/2021 majira ya usiku kimevamiwa na Simba na wananchi wa Kijiji hicho walitoa taarifa kwa vyombo vya Usalama pamoja na Uongozi wa Halmashauri na kisha Ofisi ya Mkurungenzi kutuma wataalam wake toka Idara ya Mali Asili na Wanyama pori kwenda eneo la tukio.
Hata hivyo baada ya kufika eneo la tukio mambo yalikuwa ni tofauti kulingana na taarifa jinsi ilivotolewa kwani Mwananchi aliepiga Simu na kusema kuwa ameuwa Simba wawili aliikana taarifa yake na kusema kuwa alitoa taarifa hiyo ya uwongo ili vyombo vya Usalama vifike kwa wakati hivyo basi katika mahojiano hayo taarifa ya uwepo wa Simba hao na tukio walilofanya la kuua Ng'ombe 1 na kujeruhi wengine wawili hakika ni la kweli utata ulionekana kwenye kusema Simba wawili nao wameuwawa Ndugu Roketi Mahega ni Mwananchi wa Kijiji cha Iharara ndie alietoa taarifa hizo za uwongo kuwa ameuwa Simba wawili.
Baada ya ukaguzi katika maeneo ya Pori la Kijiji Maafisa Usalama walijiridhisha kuwa Simba hawapo hivyo walifanya mahojiano ya kina na mtoa taarifa na kisha kumchukua kwa ajili ya kutoa maelezo zaidi Kituoni Mugumu huku wakiacha maelekezo kwa Wananchi kutoa Taarifa za Uhakika kuanzia kwa Ngazi ya Kijiji,Kata na Tarafa.
Imetolewa
Afisa Habari-Mahusiano
Emmanuel Isyaga Mwita
Halmashauri ya Wilaya Serengeti
tembelea:- www.serengetidc.go.tz
instagram: halmashauriwilaya
facebook : Halmashauri ya Wilaya Serengeti
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti