• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

HWGT SERENGETI YAWAHIMIZA WASICHANA KUPAZA SAUTI ZAO KETETEA HAKI ZAO

Imewekwa: October 9th, 2022

KUELEKEA  siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike  Oktoba 11, 2022  Wasichana waliokimbia ukeketaji na ndoa za utotoni wanaopatiwa hifadhi katika kituo cha 'Nyumba Salama' Kilichopo  Kiabakari Wilayani Butiama  na 'Hope Mugumu' Wilayani  Serengeti Mkoani Mara Wamewahimiza  wasichana na Wanawake wanaofanyiwa vitendo vya kikatili  kujitokeza  kupaza sauti zao kuripoti  katika Mamlaka za serikali.


Ambapo hatua hiyo  itawezesha hatua kuchukuliwa  dhidi ya  wahusika wa vitendo hivyo,  badala ya kukaa kimya na kuviona vitendo hivyo kama Sehemu ya maisha yao.


Ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya kimataifa  ya mtoto wa kike kwa mwaka  2022 inasema  'Haki zetu ni hatima  yetu wakati ni sasa'. Ambapo  siku hiyo ilipangwa na umoja wa mataifa katika kuendeleza harakati za usawa wa Kijinsia na kuongeza uwezo wa Watoto wa kike pamoja na haki zao Kama vile usawa wa Kijinsia, haki ya elimu, haki ya kulindwa dhidi ya ubaguzi, haki ya matibabu kuepushwa na ndoa za lazima.



Pia, siku hiyo huelezea mafanikio ya Watoto wa kike na Wanawake  kwa ujumla na kwa  mara ya kwanza iliadhimishwa oktoba 11, 2012.




Wamesema kutowaripoti wanaofanya vitendo vya kikatili  ni kuwapa mwanya waendelee kufanya hivyo  kitendo ambacho kina madhara makubwa na kina athiri maendeleo na ustawi bora katika  jamii. Na  hivyo, wamesisitiza  serikali kuendelea kutoa adhabu kali kwa wote wanaobainika sambamba na wadau na jamii kuendelea kukemea vikali suala la ukatili wa kijisia.




Wameyasema hayo  oktoba 9, 2022 wakati wa  mdaharo uliofanyika katika kituo cha  Hope Mugumu Nyumba Salama  kilichopo eneo la misitu Wilayani Serengeti ambapo   uliandaliwa na Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania na kuwakutanisha wasichana kutoka vituo viwili vinavyomilikiwa  na Shirika hilo ambavyo hutoa hifadhi kwa wasichana hao.






Solea Marwa kutoka Nyumba Salama

Kiabakari  Butiama amesema wapo Watoto wa kike ambao wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa Kijinsia na ndugu zao wa karibu  katoka  katika famia zao lakini wamekuwa wakiogopa kuripoti katika vyombo vya sheria ikiwemo Polisi, Dawati la Jinsia na Ofisi za serikali za mitaa wakiogopa laana. Hivyo amewaomba kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa hizo bila kuogopa.




Sarah Zabron Kutoka Nyumba Salama Butiama amesema Jamii imekuwa ikimchukulia mtoto wa kike kama chombo duni na mtu asiyethaminika  sawa na mtoto wa kiume, ameiomba serikali kuendelea kusimamia kikamifu sheria ya mtoto sambamba na kumlinda na kusikiliza malalamiko ya Ukatili pindi wanapoyatoa badala ya kukaa kimya na kuona kama sehemu ya maisha yao.





Zawadi Richard amesema mila ya ukeketaji imeendela kuwa na madhara makubwa kwa wasichana ikiwemo kutokwa damu nyingi, kuwaathiri kisaikolojia na hivyo ameomba ngariba ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya ukeketaji wapewe adhabu kali wanapotiwa hatiani ili kutoa fundisho kwa wengine wanaotamani kuketa Watoto wa kike ili kuwaozesha kwa ajili ya kujipatia kipato kinyume cha sheria za nchi.





Amina Ramadhani  Kutoka Hope Mugumu amesema kuwa Jamii inapaswa kuwapa haki ya elimu Watoto wa kike sawa na Watoto wa kiume kwani ni msingi wa maendeleo na kuimarisha usawa Katika jamii, badala ya kuwaozesha katika umri mdogo na hivyo kukatishwa ndoto zao.




"Naomba pia suala la ushahidi mahakamani lipewe mkazo kwani wakati mwingine binti anaweza kukeketwa lakini kesi inapofika mahakamani watu wahajitokezi kutoa ushahidi hili nalo ni tatizo kubwa na pia pawepo mazingira mazuri ya mtoto wa kike aliyefanyiwa ukatili kutoa ushahidi wake na alindwe vizuri." amesema Amina.






Beatrice Yohana Kutoka Nyumba Salama Kiabakari Wilayani Butiama,  amesema

Watoto wa kike wanapotimiziwa haki za msingi wanakuwa na hatima njema  kwa siku za usoni na kuisaidia Jamii kuiletea mabadiliko chanya ya kiuchumi na kijamii ambapo amesema juhudi za kupambana na vitendo hivyo zifanywe na watu wote badala ya kuichia jukumu hilo Serikali na mashirika.





Fenanzia Mwita kutoka Hope Mugumu  ameomba Viongozi wa dini kukemea vikali vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa kutoa mafundisho ya kiroho na kuonesha namna ambavyo vitendo hivyo ni dhambi kubwa na havipaswi kufanywa kwani vinakiuka maagizo ya Mungu.




Neema Chacha amewashauri viongozi wa vyama vya siasa kuwasehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wa mapambano ya ukatili wa Kijinsia kwa kukea na kuwafichua wanaofanya vitendo hivyo bila kuwaficha. Na kwamba mila na desturi zilizopitwa na wakati ikiwemo ukeketaji, ndoa za utotoni ziachwe na badala yake mila na desturi nzuri ziendelezwe kwa manufaa ya Jamii na taifa pia.



Rebeka Joshua ameomba elimu ya kupinga ukatili wa Kijinsia iendelee kutolewa hasa maeneo ya vijiji ambako Wananchi wengi hawana ufahamu na uelewa wa haki za binadamu kwa kuwafikia wazee wa Kimila na makundi mbalimbali ambayo yakielimishwa yatakuwa na mchango mkubwa wa kufanikisha mapambano hayo.




Mchungaji Steven Kolokoni wa Kanisa la  Shekinah Presbyterian Serengeti amelipongeza Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania kwa kuendelea kuwasaidia Watoto wa kike ikiwemo kuwapa hifadhi wanapo kimbia ukatili kutoka katika fanilia zao na kuwaendeleza kifani na kitaaluma ambapo amesema kitendo hicho kinawawezesha kutimiza ndoto zao. Huku akisisitiza serikali kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na mashirika na wadau wanaopambana na ukatili wa Kijinsia.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti