Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti wamewatakia kheri katika vituo vyao vipya vya kazi mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Serengeti Dkt. Emiliana Donald ambaye amehamishiwa Mji wa Kondoa Mkoani Dodoma na Mkuu wa kitengo cha manunuzi Ndg Emmanuel Kibona, ambaye amehamishiwa wilaya ya ushetu Mkoani Shinyanga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Ndg Kivuma H.Msangi amewepongeza watumishi hao kwa kufanya vizuri katika utumishi wao wilayani Serengeti
‘’Sisi tumeridhika na uwepo hapa,nendeni mkafanye zaidi mkatumie taaluma na uezoefu mliona nao vema aidha mkawe mabalozi wazuri wa serengeti ‘’Amesema Msangi
Wajumbe wa CMT wamewapongeza watumishi hao kwa namna walivyoweza kutoa mchango mkubwa katika kuijenga wilaya ya Serengeti na Taifa kwa ujumla aidha wamempongeza Mkurugenzi mtendaji kwa kuendelea kuhimiza umoja a mshikamano baina ya watumishi
Kwa wakuu wa idara waliohama wameishukuru timu ya usimamizi ya Wilaya (CMT) inayoongozwa na mkurugenzi mtendaji wa Wilaya kwa ushirikiano na umoja walio uonyesha na kuahidi kufuata mawaidha na nasaha zote walizopewa.
Hivi karibuni pia CMT na watumishi wa wilaya ya Serengeti iliagana na afisa mapato wake Ndg. Teri Hurson aliyehamia wizara ya elimu.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti