• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

GRUMETI FUND YAZINDUA MRADI WA NG'OMBE WA MAZIWA SERENGETI , BUNDA WA MIL. 52.

Imewekwa: March 8th, 2024

Kampuni ya Grumeti Fund imetoa ng'ombe wa maziwa 15 wenye thamani ya Mil. 52 kwa vijiji vya Motukeri na Nyichoka wilayani Serengeti na vijiji vya Mugeta na Tingirima wilayani Bunda,ikiwa ni awamu ya kwanza ya mradi huo unaolenga kuhamasisha ufugaji wenye tija na unao tunza mazingira.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti Fund Bi. Frida Mollel amesema lengo la mradi huo ni kuondoa changamoto za kimazingira na mabadiliko ya tabia ya tabia nchi sambamba na kuhamasisha ufugaji wenye faida na kuongeza kipato na lishe Bora katika kaya.


"Mradi huu uliobuniwa na Grumeti Fund unalenga kupunguza changamoto za kimazingira kwakuwa na ufugaji wenye tija kwa kutumia nafasi ndogo lakini matunda yake ni makubwa na wanufaika wa mradi huu wapo 15 ambao 8 ni kutoka vijiji vya Serengeti na wananchi 7 wakitoka katika vijiji vya Wilaya ya Bunda" alisema Bi. Frida


Aidha Bi. Frida amesisitiza utunzaji wa ng'ombe hao sambamba na kuzingatia taratibu za mradi ili kuufanya kuwa endelevu na wenye manufaa kwa wananchi wengi.

Bi. Frida Mollel Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Grumeti Fund akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyichoka waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Ng'ombe wa maziwa.

Vilevile, ameongeza kuwa Ng'ombe wote 15 wanamimba na wamepatiwa chanjo muhimu, ambapo pia Grumeti Fund imetoa mbegu za majani ya malisho kwa wanufaika wote ili kuhakikisha upatikanaji wa malisho kwa mwaka mzima.


Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji  amewataka wananchi kuzingatia taratibu zote za mradi na kuwataka kuutumia mradi huo kama darasa la mabadiliko kuachana na ufugaji holela na kuingia katika  ufugaji wa kisasa.

Mkuu was wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyichoka waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Ng'ombe wa maziwa.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney amewataka wanufaika wa mradi huo kuutumia vizuri ili kujikwamua katika umasikini kwa kupitia mazao yatakoyopatikana katika ng'ombe hao huku akiwataka wanufaika wa mwanzo kuwa chachu ya ushawishi kwa taasisi ya Grumeti  Fund kuleta Mradi wa awamu ya pili.

Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Anney akizungumza na wananchi wa Mugeta waliojitokeza wakati wa ufunguzi wa Mradi wa Ng'ombe wa maziwa.


Sambamba na hayo, baadhi ya wanufaika wa mradi huo wameeleza shukrani zao kwa Kampuni ya Grumeti Fund huku wakiutaja Mradi huo kama chanzo cha kukata mnyororo wa umasikini katika familia zao na kuahidi kuwatunza ng'ombe hao ili kuongeza idadi ya wanufaika.


Kampuni ya Grumeti Fund katika awamu ya kwanza ya Mradi imetoa ng'ombe kwa Wananchi  15 huku katika awamu ya pili wakitarajia kutoa ng'ombe 15, awamu ambayo itategemea mafanikio yatakayopatikana katika awamu ya Kwanza.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti