Kampuni ya Grumeti Fund kupitia Idara ya maendeleo ya Jamiii imewakumbusha vijana wa kiume Wilayani Serengeti kutekeleza majukumu yao katika jamii zinazowazunguka.
Akizungumza katika Kongamano la vijana wa kiume lilofanyika leo tarehe 25 Machi 2023 waliotoka shule za Sekondari Serengeti na Nyichoka Mgeni Rasmi Mwl.Rwakatare amewakumbusha vijana hao kuhakikisha wanatelekeza wajibu wao ipasavyo katika jamiii ikiwemo kuwalinda na kuwapa vipaumbele vijana wa kike sambamba na kujiisamamia ili waweze kutimiza ndoto zao.
"Vijana wa kiume tunawajibu wa kutimiza ndoto zetu,Lakini pia tunawajibu wa kuhakikisha kwamba binti unayeishi naye Katika jamii yako naye anatimiza ndoto zake,elimu unayoipata ikusaidie kuionyesha jamii ambayo unaishi nayo kwamba tunazo mila ambazo zinamkandamiza mtoto wa kike ambazo kwa sasa azisitahili’’ amesema Mwl.Rwakatare
Mwl.Rwakatare aliongeza kwa kusema pia mabinti katika ngazi za elimu ya chini hawafanyi vizuri kutokana mikandamizo ambayo tunayo katika jamii,lakini mtu ambaye anastahili kumlinda huyo binti ni wewe kaka yake,wewe ni jeshi linalomzunguka binti,uwe askari wake akiwa shuleni ,nyumbani au Njiani ili tunapotakana kufikia ndoto zetu tufikie kwa pamoja’’.
Kwa upande wake Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamiii wa Kampuni ya Grumeti Fund Frida mollel amewasihi Vijana hao kuwasehemu ya mabadiliko chanya katika kutimiza majukumu yao
‘’Wanaume wana Nguvu Kubwa sana katika agenda ya kumuwezesha binti kufikia ndoto zake kuanzia mdogo,Mashuleni,Makazini lakini pamoja na majumbani,Tupige vita mila na desturi zisizo na tija’’
Frida ameongeza pia badala ya mtoto wa kiume na kike kushindani kusiwepo bali kuinuana ili kwenda sambamba,mkatekeleze yote mliyojifunza kwenye kongamano hili’’
Nao vijana walioshiriki katika kongamano hilo wameishukuru Kampuni ya Fund kwa kutoa elimu na kuahidi kuwa mabalozi wazuri na kutekeleza yote waliyoelekezwa katika kongamano hilo.
Kongamano hilo lilofanyika katika shule ya sekondari serengeti limewafikia Vijana wa kiume 416 ,ambapo Jezi na mipira kwa timu kutoka shule za sekondari nyichoka na Serengeti zilitolewa,Aidha vijana hao walishiriki katika Michezo mbalimbali ikiwemo Mpira Miguu,kukimbiza yai kwenye Kijiko ,kukimbia kwenye viroba na Zawadi kwa washindi kutolewa.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti