• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

GRUMETI FUND YATOA ELIMU YA KIJINSIA KWA WANAFUNZI ZAIDI YA 1,000 SERENGETI NA BUNDA.

Imewekwa: May 28th, 2024

SHIRIKA la Grumeti Fund  kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imewaleta pamoja Wanafunzi wa kike 704 na wakiume 634 kutoka katika shule za Tirina,Chamriho na Hunyari Wilayani Bunda, kwa lengo la kutoa Elimu sambamba na kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili watoto wa kike na kiume ili kujenga jamii yenye usawa na yenye kujitambua  kwa vijana wa jinsia zote.

Katika kongamano la wasichana lililofanyika katika shule ya Sekondari Hunyari iliopo Wilayani Bunda Mkoani Mara, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti Fund Bi. Frida Mollel amesema  lengo la Grumeti Fund kufanya kongamano hilo ni kuwaelimisha watoto wa kike kutambua thamani yao sambamba na kuwajengea uwezo wa kujiamini na kufikia ndoto zao.

"Kutokana na utafiti tulioufanya juu ya uchache wa watoto wa kike katika kuchangamkia fursa za kimasomo zinazotolewa na Grumeti Fund, moja ya njia za kutatua changamoto hii ni kufanya makongamano kwa nia ya kutoa elimu kwa mabinti, kwanza wafahamu thamani yao na pili wafahamu kwamba wanaweza kuwa mtu yeyote watakae katika maisha yao  na kukataa kukatishwa tamaa na mtu yeyote. Nataka mfahamu kwamba mnaweza"

Aidha, Bi. Frida amewataka wasichana hao kutokata tamaa kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili bali watumia elimu wanayoipata ili iweze kuleta tija na mabadiliko chanya katika jamii na kusisitiza kuwa elimu ndio dira na njia ya kufikia ndoto za vijana hao.

Katika kongamano hilo shirika la Grumeti Fund imetoa msaada wa taulo za kike  zinazoweza kutumika  kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu (reusable pads) kwa wanafunzi wa kike 704 zenye thamani ya Shilingi Milioni tisa laki nane na elfu hamsini na sita (9,856,000) katika shule za sekondari Tirina,Chamriho na Hunyari

Naye mgeni rasmi katika katika kongamano hilo, Neema Paul ambaye ni Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amewataka wasichana kuzingatia nidhamu sambamba na kuweka malengo katika masomo yao ili waweze kufanikiwa huku akiwataka kutokata tamaa katika masomo yao

"Mwanafunzi yeyote yule unatakiwa kuwa na malengo,hujaja shuleni kutembea Wala kukua weka malengo kuwa unataka kuwa nani na hakikisha unapambania malengo yako kwa kuweka mikakati sahihi" Alisema Bi.Neema

Kwa upande wake  mkufunzi kutoka  chuo cha Afya Kisare Mwl. Restuda Murutta amewaasa wanafunzi hao kuzingatia elimu ya afya ya uzazi sambamba na kuepuka vishawishi vitakavyo waingiza katika kufanya mapenzi katika umri mdogo na mwisho kupelekea ndoa za utotoni.

“Inasikitisha binti anaumri chini ya miaka 18 ameshaanza kujiingiza kwenye mahusiano ya ngono kitu ambacho sio salama, kabla ya kuingia kwenye mambo hayo kwanza jiulize je ni umri sahihi wa kuingia kwenye Mambo hayo ukishapata jibu acha" alisema Bi. Restuda

Nao miongoni mwa wanafunzi waliopata mafunzo hayo ameishukuru kampuni ya Grumeti Fund kwa namna wanavyowajali na kuwathamini mabinti  na kuahidi kuyaweka katika vitendo mafunzo hayo na kusambaza elimu kwa wengine.

Awali kongamano hili lilitanguliwa na kongamano la vijana wa kiume takribani 634 kutoka shule za Sekondari Tirina,Chamriho na Hunyari ambapo Bi. Frida Mollel Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya jamii kutoka Grumeti Fund amesema baada ya jamii kuwekeza nguvu kubwa katika kutoa Elimu kwa watoto wa kike imefanya watoto wa kiume kusahaulika ndipo Grumeti Fund katika kuleta usawa katika hilo ikaamua kuanzisha makongamano kwa watoto wa kiume ili kujenga jamii shirikishi na yenye usawa na kawaasa vijana kutokuiga tabia na tamaduni za kigeni zinazoweza kuharibu kabisa thamani yao na maisha yao kwa ujumla sambamba na kushiriki katika kutokomeza Mila na desturi kandamizi kwa watoto wa kike.

Naye aliyekuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo Ndg. January Kizumba ambaye ni Afisa Elimu Sekondari kwa upande wa taaluma kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda akawataka vijana wa kiume kusisitiza usawa katika jamii sambamba na kuwekeza nguvu katika masomo yao ili kuleta mapinduzi katika jamii.

 "Nyie ndio kizazi Cha kesho hivyo tunatarajia,ili tuwe na jamii yenye usawa ni lazima tuwaelimishe pande zote mbili ili muwe na uelewa juu ya Mambo yakijisia maana yake tutajenga jamii endelevu na yenye usawa" Alisema Kizumba

Kwa takribani miaka saba kampuni ya Grumeti Fund imekuwa ikitoa elimu ya kijinsia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za sekondari mbalimbali Wilayani Serengeti na Bunda ambapo tangu mwaka 2017 hadi awamu hii ya pili  ya kongamano hili kwa Mwaka 2024  imefanikiwa kutoa elimu ya kijinsia kwa wasichana 11,796 na kutoa taulo za kike kwa kila binti anayeshiriki mafunzo hayo, huku ikifanikiwa kutoa mafunzo kwa wavulana zaidi ya 4,629 tangu mwaka 2021 hadi awamu hii  ya kongamano la Mwaka 2024 na kutoa zawadi za jezi na mipira  kwa kila shule iliyoshiriki kwenye kongamano.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti