• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

GRUMETI FUND YAJIVUNIA KUWAFIKIA VIJANA ZAIDI YA ELFU 20 MKOANI MARA.

Imewekwa: November 3rd, 2024

SHIRIKA la Grumeti Fund kupitia Idara ya Maendeleo ya jamii limejivunia mafanikio yake katika kutoa elimu ya kijinsia kwa vijana wa kike na wa kiume zaidi ya elfu 20 katika Wilaya za Serengeti na Bunda Mkoani Mara jambo linalosaidia kujenga jamii yenye ushirikiano wa pamoja kati ya vijana wa kike na kiume na hatimae kujenga jamii yenye usawa miongoni mwa vijana wa jinsia zote.

Kwa takribani miaka saba Shirika hilo limekuwa likitoa elimu ya kijinsia kwa wanafunzi wa kike na kiume katika shule za sekondari mbalimbali Wilayani Serengeti na Bunda ambapo tangu mwaka 2017 hadi kufikia Mwaka huu 2024  limefanikiwa kutoa elimu ya kijinsia kwa wasichana 15,352 na kutoa taulo 15,352 kwa kila binti anayeshiriki mafunzo hayo, huku ikifanikiwa kutoa mafunzo kwa wavulana zaidi ya 7,473 tangu mwaka 2021 hadi mwaka huu 2024 na kutoa zawadi za jezi na mipira  kwa kila shule iliyoshiriki kwenye kongamano.

Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Grumeti Fund Bi. Frida Mollel akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha wageni kutoka nchi mbalimbali waliotembelea Shirika la Grumeti Fund kama hatua ya kushuhudia na kuunga mkono jitihada za Shirika hilo katika kuwapa mabinti elimu ya kujitambua maarufu kama (SERENGETI GIRLS RUN) amesema wageni hao wamekuja kuunga mkono jitihada za Grumeti Fund ili kupata nguvu zaidi na kutanua wigo katika kumkomboa mtoto wa kike katika maeneo mbalimbali hususani katika kupata haki ya elimu na mahitaji muhimu wakati wa hedhi.


Aidha Bi. Frida ameongeza kuwa Grumeti Fund inajivunia makongamano mbalimbali ambayo yamekuwa yakifanywa na Shirika hilo kwani yameonesha mabadiliko makubwa katika jamii sambamba na kuwapa nguvu watoto wa kike na wa kiume katika kupambania ndoto zao na kubadili mitazamo hasi katika jamii na kutoa wito kwa jamii kuzingatia usawa baina ya mtoto wa kike na wa kiume ili kujenga jamii endelevu na yenye usawa.

"Grumeti Fund imekuwa ikiongea na kutoa fursa kwa  vijana kushiriki kutoa mawazo yao ni kwa jinsi gani wanaweza kuzishinda changamoto zinazowakabili. Tumekuwa  tukiwashauri na kuonesha umuhimu wao katika jamii ili waje kuwa kizazi bora kwani tunaamini kwamba jamii yenye usawa ndani yake ni jamii yenye maendeleo, leo mabinti wameonesha jinsi ambavyo wamenufaika na semina zetu, wameonesha nguvu na ujasiri hivyo natoa wito kwa Jamii kumchukulia mtoto wa kike sawa na wa kiume kwamba wote wanastahili kupendwa na kupewa nafasi ya kupata elimu tusiwe na tabia ya kubagua watoto" alisema Bi. Frida

Kwa upande wa wanafunzi wa kike walioshiriki hafla hiyo wameeleza mafanikio makubwa waliyopata kupitia semina mbalimbali ambazo zimekuwa zikitolewa na Grumeti Fund na kueleza namna ambavyo zimebadisha fikra zao na kuamsha ari na ujasiri katika kupambania ndoto zao na kuhamasisha usawa katika jamii.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU. March 07, 2025
  • TANGAZO LA KUTOA MAONI KUHUSU SHERIA NDOGO. February 24, 2025
  • TANGAZO KWA UMMA January 02, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SIKU YA MALARIA WILAYANI SERENGETI

    April 25, 2025
  • KAMATI YA FEDHA UONGOZI NA MIPANGO WATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA.

    April 16, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI SERENGETI LAPITISHA BILIONI 48.8 KAMA MPANGO WA BAJETI YA HALMASHAURI 2025/2026.

    March 04, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI WILAYANI SERENGETI LAPITISHA MPANGO WA BAJETI YA TARURA BILIONI 2.4

    March 03, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti