Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg. Afraha N. Hassan ametembelea Zahanati ya Kono iliyopo Kata ya Nata ambayo imeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Serengeti.
pamoja na kutoa pole kwa wananchi wa kata hiyo Ngh. Afraha amechangia kiasi cha shilingi Milioni moja ili kuwezesha ukarabati wa zahanati hiyo na kuwataka kuharakisha jambo hilo kabla ya kutokea uharibifu zaidi unaoweza kusababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha.
Aidha amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchukua taadhali za mvua ili kuepuka madhara zaidi yanayoweza kuletwa na mvua hizo.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti