Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Ndg.Afraha Hassan,amewashukuru wadau wa maendeleo Wilayani Serengeti Benki ya Azania Kwa Kutoa msaada wa Mapipa ya kuhifadhia taka.
Aidha, Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Serengeti ametoa wito Kwa wadau wengine wa maendeleo kujitokeza katika kutoa misaada mbalimbali.
Kwa upande wa Afisa Mdhibiti wa taka na usafi wa Mazingira(W) Ndg.Ezekiel Gamaya amewahasa wananchi kuendelea kujitokeza kushiriki kwenye usafi wa Mazingira hasa katika kipindi hiki ambapo ulimwengu una azimisha wiki ya usafishaji ambapo tarehe 16/09/2023 ndio itakua kilele na wananchi tutashiriki Kwa kufanya Usafi katika maeneo yanayowazunguka.
Naye Meneja wa Bank ya Azania Bi.Elizabeth koboko alisema wamewiwa kutoa msaada ingawa ni kidogo Kwa kuanzia wanajipanga Kwa bajeti ijawayo wataongeza kiwango.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti