Mkuu wa wilaya ya Serengeti Dkt. Vincent Mashinji amewataka Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuhakikisha visima vyote vya umma na binafsi vinatoa maji yaliyotibiwa sambamba na kuhakikisha ukaguzi wa visima hivyo kabla ya kutoa leseni.
Dkt. Mashinji ameyasema hayo katika Mkutano wa RUWASA na Wadau wa sekta ya maji uliofanyika katika ukumbi wa Giraffe Wilayani Serengeti ambapo amesema RUWASA kabla ya kutoa leseni za visima ni lazima visima hivyo viwe vimekaguliwa na kuwekewa dawa ili vitoe maji Safi.
'"Tumewaelekeza RUWASA kuhakikisha ukaguzi wa visima kabla ya kutoa leseni na viwekewe dawa kuhakikisha kwamba yale maji yanayotoka kule ndani ni salama" alisema Dkt. Mashinji.
Aidha Dkt. Mashinji ameagiza Kaya zote Wilayani Serengeti kuhakikisha zinakuwa na vyoo sambamba na kuzingatia matumizi ya vyoo hivyo ili kuepuka uwezekano wa kuibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu.
"kila Kaya lazima iwe na choo bila kujali Mila na desturi zenu, kuchimba ni Jambo moja na kutumia ni jambo lingine kwahiyo maelekezo ni kuchimba na kutumia choo" aliongeza Dkt. Mashinji.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti