Mkuu wa Wilaya mpya wa Serengeti Mhe. Angelina Marco Lubela amekabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Kemirembe Lwota katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi wa Chama na Serikali katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Serengeti.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mhe. Angelina amemshukuru Mwenyenzi Mungu kupitia Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa imani yake kubwa na kumpa dhamana ya kuongoza Wilaya ya Serengeti na kumshukuru Mtangulizi wake Bi. Kemirembe kwa kazi kubwa aliyoifanya katika Wilaya ya Serengeti kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Zaidi amewataka watumishi wa Umma kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kwa kusimamia Kanuni, Sheria na taratibu kwa kutoa huduma bora na kwa wakati kwa wananchi wote, ili kila mtua aweze kufurahia matunda ya Serikali na nchi yake.
Awali Mhe. Angelina alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Serengeti kabla ya kuteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Juni 23, 2025.
Mhe. Angelina katika historia ya Wilaya ya Serengeti anakuwa mwanamke wa pili kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo baada ya mtangulizi wake Bi. Kemirembe Lwota.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti