Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Ndg.Patrick Chandi amewapongeza wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kusimamia Na kutelekeza vema ilani ya Chama Cha Mapinduzi na kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassani.
‘’Niwapongeze sana kwa kuwatumikia vema wananchi wa wilaya ya Serengeti, kupitia utekelezaji wa ilani Makini ya Chama cha mapinduzi,mzidi kuchapa kazi na kama kuna changamoto yoyote inayowakwamisha katika utekelezaji wa majukumu yenu nishirikisheni’’amesema Chandi
Ameongeza pia,menejimenti inaendelee kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na umoja baina ya watumishi pamoja na kuwashauri vizuri madiwani ili kuzidi kuleta ufanisi katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi (CCM).
Kwaniaba ya Menejimenti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti Ndg.Kivuma H.Msangi amempongeza Ndg.Chandi kwa kuaminiwa na wana CCM mkoa wa Mara kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa na kumuahidi ushirkiano.
‘’Timu hii itahakikisha inafanya kazi vizuri na wewe ili kuiletea maendeleo wilaya yetu ya Serengeti na Kuendelea kukushirikisha katika maswala mbalimbali yahusuyo wilaya yetu’’amesema Msangi.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti