Watumishi wa idara ya afya katika Wilaya ya Serengeti wametakiwa kutoa bure huduma za matibabu kwa wazee wenye miaka zaidi ya 60 walio na vitambulisho.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akitoa kitambusho kwa Mzee johannes Magaigwa Chacha.
Agizo hilo limetolewa na jana tarehe 18 Januari 2018 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipokuwa akikabidhi vitambulisho 280 kwa wazee ili kupatiwa huduma za matibabu popote katika zahanati, vituo vya afya na hospitali ndani ya Wilaya ya Serengeti.
“Nawapongeza Serengeti kwa kutekeleza kwa vitendo agizo hili la Rais, Mheshimiwa Magufuli la kutaka wazee wenye umri kuanzia miaka 60 watibiwe bure” alisema Mheshimwia Majaliwa na kuendelea kwa kusema “Natoa agizo kwa watumishi wa afya kuwahudumia bure wazee wenye vitambulisho hivi na msiwatoze fedha yoyote”
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa hospitali ya WIlaya Serengeti.
Awali Mheshimiwa Majaliwa alipata nafasi ya kukagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya inayojengwa katika eneo la Kibeyo nje kidogo ya Mji wa Mugumu Serengeti na kupokea taarifa ya ujenzi wa hospitali hiyo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Nurdin Babu.
“Kwa muda mrefu sasa ujenzi wa Hospitali ulikuwa umesimama, kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini, tuliunda kamati maalumu iliyohusika na uhamsishaji wa ujenzi wa hospitali hii na kupitia kampeni ya Jenga Hospitali kwa shilingi elfu moja (1000) pamoja na kufanya harambee tumepata fedha za ujenzi wa hospitali hii mpaka hatua hii unayoiona sasa”
Waziri Mkuu alionyesha kuguswa na jitihada za ukamilisahji wa Hospitali hiyo na kuahidi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 10 za kitanzania kuunga mkono. Aidha katika harambee iliyofanyika hospitalini hapo raia mwema mwenye mapenzi na Wilaya ya Serengeti Bwana Adrea nyantori alitoa fedha taslimu shilingi milioni kumi papo hapo kuunga mkono huku jumla ya shilingi milioni thelathini na moja na elfu hamsini (31,050,000/=) zilichangwa pamoja na ahadi za mifuko mia sita na tano (605) ya saruji kutoka kwa wadau wa maendeleo.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni 10 (mchango wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Serengeti) toka kwa Bwana Andrea Nyantori.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa akiteta jambo na Bwana Andrea Nyantori.
Mheshimwa Babu hakusita kumuomba Mheshimwa Majaliwa kuisaidia Wilaya ya Serengeti kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo kwa kuipigia chapuo ili iweze kupatiwa fedha na Serikali kuu huku akitarajia huduma kuanza kutolewa mwishoni mwa mwezi februari mwaka 2018.
Kaimu Mganga mkuu Wilaya ya Serengeti Daktari Deo Kisaka akimuonyesha Mheshimiwa Majaliwa mchoro sanifu wa hospitali ya Wilaya ya Serengeti
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti