• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Malalamiko na Mrejesho |
    • Barua pepe za watumishi |
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Malengo
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha & Biashara
      • Afya
      • Kilimo,Ushirika na Umwagiliaji
      • Ujenzi & Zimamoto
      • Maendeleo Ya Jamii
      • Mazingira & Usafishaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • MIfugo & Uvuvi
      • Ardhi & Maliasili
      • Water
    • Vitengo
      • TEHAMA & Uhusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Nyuki
      • Ukaguzi wa Ndani
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Water
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu.
    • Ratiba
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Fomu Mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Ripoti Mbalimbali
      • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Video

GIZ wamimina misaada Serengeti DC

Imewekwa: January 30th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kupitia Idara ya Ardhi na Maliasili imepokea msaada wa pikipiki tano (5) pamoja na vifaa vya tehama vyote vyenye thamani ya shilingi 43,521,000/= kutoka Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ)

Makabidhiano ya pikipiki na vifaa hivyo yamefanyika jana tarehe 29/01/2018 katika ofisi za Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambapo Bi Dagmar Wittine (Mshauri wa Maendeleo) kutoka shirika la GIZ alikabidhi rasmi vifaa hivyo vilivyopokelewa na watumishi kwa mikono miwili.  Bi. Dagmer hakusita kusisitiza juu ya matumizi bora ya vifaa hivyo na kuwataka watumishi wenye uhaba wa vitendea kazi kutuma maombi ili waone namna ya kuisaidia Halmashauri. Aliendelea kwa kusema “Tulipokea maombi ya kusaidia ununuzi wa pikipiki na vifaa hivi kutoka Idara ya ardhi na maliasili mwaka jana (2017) na leo tuko hapo kwa ajili ya kukabidhi vifaa hivyo”

 Kupitia msaada huo kutoka Shirika la GIZ sasa watumishi toka Idara ya Ardhi na Maliasili wanatarajiwa kuboresha zaidi utendaji kazi kwa ufanisi na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mheshimiwa Juma Porini amewashukuru GIZ kwa kuendelea kuijengea uwezo Halmashuari na kuwaomba kutosita kutoa misaada zaidi pindi inapohitajika. Mheshimiwa Porini pia alisisitiza juu ya matumizi ya pikipiki na vifaa hivyo ili kuleta tija, kwa kusema “Tunakazi kubwa huko vijijini, hivyo pikipiki hizi zitumike katika kazi ya upimaji wa vijiji 36 na natarajia kuona tunakamilisha kazi  hiyo kwa wepesi na ufanisi zaidi”

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Dickson Kamazima amesisitiza juu ya matumizi bora ya vifaa hivyo kuleta tija na kuwataka watumiaji wa vifaa hivyo kuvitumia kwa umakini na uangalifu zaidi.

Huu ni mwendelezo wa misaada inayoendelea kutolewa na shirika hilo la GIZ ambapo watumishi kutoka idara mbalimbali katika Halmashauri wametakiwa kuandika maandiko miradi ili kuweza kupata misaada toka GIZ.

Matukio katika picha

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mhandisi Dickson Kamazima (kushoto) akipokea hati ya makabidhiano toka kwa Bi Dagmar Wittine (Kulia) Mshauri wa Maendeleo GIZ.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Mheshimiwa Juma Porini (Kushoto) akisalimana na Bi Dagmar Wittine.

Vifaa vya tehama walivyopatiwa Idara ya Ardhi na Maliasili.

Bi Dagmar akitoa bahasha zenye funguo za pikipiki kwa Watumishi wa Idara ya Ardhi na Maliasili.



Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA September 16, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI July 01, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SERENGETI. June 11, 2025
  • ORODHA YA MAJINA WALIOITWA KWENYE MAFUNZO YA UBORESHAJI WA DAFTARI AWAMU YA PILI KWA WAENDESHA BVR NA WAANDISHI MSAIDIZI April 28, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI AMTAKA MKANDARASI KUONGEZA NGUVU YA UTEKEKEZAJI WA MRADI WA MAJI SERENGETI.

    September 13, 2025
  • RC MTAMBI, AWAKARIBISHA WANANCHI KWENYE MAADHIMISHO YA MARA DAY.

    September 11, 2025
  • SEMINA YA SIKU TATU KWA WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI NGAZI YA KATA JIMBO LA SERENGETI YAHITIMISHWA RASMI.

    August 06, 2025
  • BARAZA LA MAMLAKA YA MJI MDOGO SERENGETI LAZINDULIWA LEO.

    July 10, 2025
  • Angalia zote

Video

AKINA MAMA SERENGETI WASEMA ASANTE MAMA SAMIA.
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Maktaba ya Picha za Matukio mbali mbali
  • Matokeo ya Kidato cha nne mwaka 2017
  • Bofya hapa kupata fomu mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti
  • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • UCHAGUZI KIDATO CHA KWANZA 2022 SERENGETI DC
  • FOLLOW US INSTAGRAM
  • Matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Kidato cha pili (FTNA) 2017
  • FOLLOW US TWITTER

Viunganishi Linganifu

  • Ikulu ya Rais
  • Utumishi
  • Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Sekretarieti ya Mkoa wa MARA
  • Tanzania National Parks TANAPA
  • Frankfurt Zoological Society (FZS)

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    31603 Stendi Kuu | Serengeti

    Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti

    Simu ya mezani: 0282985686

    Simu: 0782677763

    Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz

Other Contacts

   

Wageni waliotembelea tovuti

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti