Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Serengeti anapenda kuwataarifu waombaji wa nafasi za Msimamizi wa Kituo, Msimamizi Msaidizi wa kituo na Karani Muongozaji wa Kituo katika zoezi la Kupiga Kura katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani litakalofanyika Tarehe 28.10.2020 ambao majina yao yametajwa katika Tangazo hili wafahamu kuwa amewateuwa kushiriki Mafunzo kama ifuatavyo;
Hivyo kila mmoja atakayehudhuria mafunzo haya anatakiwa kuhakiki jina lake katika orodha iliyopo chini ya tangazo hili tangazo hili.
Aidha waombaji wote walioteuliwa mnajulishwa kuja na kitambulisho kimojawapo kati vya vifuatavyo; Cha kazi, cha uraia, cha mpiga kura, leseni ya Udereva au kitambulisho cha bima ya Afya
Kwa wale ambao majina yao hayajatajwa katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/Hawajateuliwa.
31603 Stendi Kuu | Serengeti
Anuani ya Posta: 176 Mugumu Serengeti
Simu ya mezani: 0282985686
Simu: 0782677763
Barua pepe: ded@serengetidc.go.tz
Hakimiliki © 2018 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti